Yahoo! 360° News | Beta Feedback
Start your own Yahoo! 360° page

MWIMBAJI WAPO

Top Page  |  Blog  |  Friends  |  Lists  |  Groups

  • Work: WAPO MISSION

Add

MWIMBAJI WAPO is not connected to you in Yahoo! 360°.

Last updated Wed Feb 15, 2006 Member since February 2006

Hakuna Lisilowezekana! Imba na mtegemee Mungu; Healing is at your door Reply

1 - 4 of 4 First | < Prev | Next > | Last

MWIMBAJI WAPO's Blog Full Post View | List View

Historia ya Mwimbaji wa Injili: Mafanikio, Mipango, Matatizo, Matarajio, Picha za matukio ya maisha

ROZI MHANDO NA BAHATI BUKUKU NI WADOGO ZANGU
ROZI MHANDO NA BAHATI BUKUKU NI WADOGO ZANGU magnify

Sasa nimeona wakina Rozi Mhando na Bahati Bukuku ni wadogo zangu kimusic, na tunaheshimiana na wananielewa. Na nikaona kwamba  ni vyema, waimbaji bado wanazaliwa ngoja na mimi nifungue studio ili nitakapozeeka.

Nami niwe na kitu cha kusema, hii ndio kazi niliowahi kufanya. Maana labda production itakwisha kwa hao Wahindi, hivyo nami nijifanyie kitu ambacho kitasaidia hii jamii ijayo. 

Katika nyimbo zangu hili ni toleo la sita (wimbo wa Yesu anaweza Yote). Matoleo manne yapo kenya, na mawili ndio yapo hapa kwetu Tanzania. Halafu kuna wimbo mwingine ambao tayari CD yake imeshatoka.

Lengo langu na mategemeo yangu ni nini? 

Wednesday February 15, 2006 - 12:46am (PST) Permanent Link | 0 Comments
NIMETIKISA SANA MWANZA !
NIMETIKISA SANA MWANZA ! magnify

Wakati niko Kenya, nilikuwa na wadhamini kutoka serikalini. Maana walia aprreciate ile kazi ninafanya, lakini unaona sanaa ya hapa kwetu Tanzania, Serikali haijihusishi sana.

Yaani hata leo ningeimba wimbo wa Tanzania, ningetunga wimbo wa kuisifu Tanzania, niipendezeshe Tanzania. Hakuna kitu watanisaidia.

Mfano maendeleo kama ya Rozi Mhando, si kuwa Serikali ndio inayomfanikisha katika matamasha yake. Anayemwandalia Rozi Matamasha ni Mama Mshama na Mshama Promotion

Kwa hiyo unakuta kwamba na mimi mwenyewe nimewahi kuandaa Matamasha. Nikamwita Rozi Mhando. Yaani hakuna. Rozi ameinuka kutokana na hawa Wahindi, hawa Wahindi Promotion yao ni nzuri.

Sasa kama ni nzuri promotion yao, unakuta kwamba ndio inayofanya tupanuke. Japo Wahindi wanatuibia sana! Yaani kama ni kutuibia wanatukwiba kweli, lakini sasa tusemeje. Kwa vile hatuna jinsi ya kuwabana. Lakini Kenya huwa kuna fungu Maalum kwa ajili ya sanaa.

Nakumbuka mimi nikiimba Kenya huwa nalipwa television ya Kenya, KBC. Hadi hivi sasa nalipwa na television ya Kenya. Yaani ndugu zangu waliobakia Kenya, wanafuatilia ni mara ngapi nimetokeza katika television ya Kenya.  Halafu wananilipa.

Sasa hivi hapa Tanzania, hutaniona nikiimba katika television ya Taifa, nikatokea kupangiwa fungu fulani na television yetu kulipwa fungu fulani. Lakini, angalia jinsi ambavyo wimbo wa Yesu anaweza yote ulivyokubalika na jamii.

Channel Ten ndio wamenisaidia kiasi, na kuna payment kidogo, hata tamasha langu la Shinyanga, onyesho la Shinyanga wao ndio wamenisaidia.

Mara nyingi lengo la Tamasha. Na tarajio langu hata ukiangalia mabango yangu ya onyesho la Kahama. Lengo la tamasha tunavyofanya, ni kwa ajili ya kufungua studio, unajua mimi ni mwimbaji mkongwe. Na ndio nilikuwa Mwanamke wa kwanza kuimba.

Nina uhakika kabisa uliza makanisa yote, hakuna mwanamke wa kwanza aliyeimba Gospel songs. Mpaka ilikuwa inanipa shida, wananiambia hatuumini uimbaji wako, wananieleza niende kwenye makanisa nijiunge na kwaya.

Kwa hiyo mimi ni wa kwanza.

 

Tuesday February 14, 2006 - 06:59am (PST) Permanent Link | 1 Comment
Serikali ya Kenya Walikubali kazi yangu
Serikali ya Kenya Walikubali kazi yangu magnify

Watoto hawa nimewafundisha vizuri na wanaweza kucheza mbele za watu wengi huku wakitifuatifua mioyo ya wasikilizaji au waumini ili kusubiri mahubiri.

Kwa jinsi walivyo na ni wakiwa (yatima) wakiimba, Mchungaji mhubiri atakuwa na kazi ndogo ya kuhubiri kwani kwa uzoefu nilionao, watoto hawa ni mahubiri tosha.

Watoto hawa si tu kuwa wanaimba na kutifua mioyo ya waumini tayari kusikiliza neno la Mungu, lakini pia wanasoma. Na ninawagharamia. Nadhani unaweza kuona ni kiasi gani mbali na wito wa kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji, lakini nina wito vilevile wa kusaidia watoto wasiokuwa na uwezo katika jamii. 

Katika watoto hao, wengine ni wa Dada mmoja ambaye alipata Mateso sana katika ndoa yake naye nimewachukua watoto wake ili kumsaidia. Mimi nimekwisha kuwa mtu wa Jamii, inabidi nikubaliane na hali halisi kama mtumishi wa watu.

Jumla ya watoto ninaoshinao ni tisa (9), watoto wangu watatu na wengine hao sita. Nimeanza kuishi nao watoto hawa toka Mwaka jana mwezi wa saba(Julai, 2004). Watoto hao baba yao alipata matatizo amewekwa ndani sasa ninawalea wote. 

Tuesday February 14, 2006 - 06:24am (PST) Permanent Link | 1 Comment
Catherine Kyambiki
Catherine Kyambiki magnify

Catherine Kyambiki: Toka hapo mwanzo nimekuwa nikiimba nchini Kenya na baada ya kuonekana naimba vizuri, nilipewa uraia na Rais wa Kenya wakati huo Mheshimiwa Daniel Arap Moi nikiimba nyimbo za serikali. 

Kwa hiyo kila sherehe za kiserikali kwa mfano Kenya Day, Kenyatta Day nilikuwa nikiimba nyimbo za sikukuu hizo. Niliendelea kumudu kuimba nyimbo hizo.

Baada ya mafanikio ya hapa na pale niliamua nirudi kwetu Tanzania, baada ya kufika Tanzania ndio nikapata wito wa kuimba nyimbo za Yesu anaweza yote. Na tokea nimerudi nimepata vilevile wito wa kusaidia watoto wasiokuwa na uwezo na kufanya kitu kinaitwa Dancer Kids(ambao hawana wazazi, au ndugu zao wananipa ili niwalee lakini nawashirikisha na watoto wangu na si wao peke yao).

Nimeshirikiana na watoto hao ambao ni yatima na ukiangalia katika CD yangu utaona ninaimba nao watoto hao ili kuwasaidia na kuwalea ili wajisikie kama watoto wenye wazazi wao na wanafanya kile ambacho wazazi wao wanafanya.

Tuesday February 14, 2006 - 05:12am (PST) Permanent Link | 0 Comments

Add MWIMBAJI WAPO's Blog to your personalized My Yahoo! page:

Add to My Yahoo!RSS About My Yahoo! & RSS
1 - 4 of 4 First | < Prev | Next > | Last